Thursday, January 31, 2019

SEBENE LA MAMA MKWE 7

SEBENE LA MAMA MKWE
7
MTUNZI. Baujiti
MAMBA. 0742868019
Endeleaaaa.....
Nilisikia mkono umenishika begani kugeuka nikakutana uso kwa uso na baba yake sophy, nilishituka nikakosa cha kuongea nikabaki namanga manga bila kuongea chochote mpala pale yeye aliponiongelesha,
"Kijana wewe ndie unaniharibia binti yangu eehhee?
"Mzee tulikuwa tunaongea tu,
"Kuongea ndio mshikane shikane hivyo?
"Mzee nisamahe,
"Nikusamehe nini?
Niliona mzee anazidi kuwa mkali na sauti yake anazidi kuipaza juu mpaka watu wakaanza kusogea sogea,
Niliona isiwe tabu nikajiuliza miguu nilipewa ya nini? Nikapata jibu nilipolipata niliona hakuna cha kusubili niligeuka kama vile nimeshituliwa baba yake na sophy aliona shati inapepea tu akashindwa afanye nini,
Nilifika kwangu moja kwa moja nikazama chumbani nikaanza kujiuliza kama baba sophy akienda polisi si watakuja kunikamatia hapa, nilipofikilia hilo nilitoka chumbani kwangu nikaingia kwenye chumba cha miraji,
"Derick vipi?.
"Poa,
"Mbona kama hauko sawa,
"Acha ndugu yangu ni majanga tu,
"Yapi tena?
"Si unajua niliwaacha pale kijiweni mimi nikashuka na yule shizo,
"Shizi yupi huyo?
"Si sophy,
"Ehee imekuwaje?
"Nilishuka naye tulipofika pale kwa mangi si nikamvutia chocho nikaanza kumtomasa tomasa eeebwanaweee yaliyonikuta ni makubwa si baba yake kanibamba,
"Mh!!!! Ikawaje sasa?
"Unauliza mkuki kwa masai nikakimbia,
"Huo ni msala mwangu,
"Sasa leo nitabana kwako hapa maana nahisi usalama haupo,
Tukiwa tunaendelea kuongea mala nikasikia mlango wangu unagongwa nikashitu,
Chumba cha miraji hakikuwa mbali na chumba changu kwani nyumba ilikuwa ni moja kwa hiyo mlango ulipogongwa mimi nilisikia vizuri,
"Derick wakati unaingia humu hao akina dada wa vyumba vingine hawajakuona?
"Hawajaniona,
"Sasa fanya hivi acha nikaangalie anayegonga hodi chumbani kwako,
"Poa,
Miraji alitoka aliporudi,
"Duuuhhh!!!! Ni nomaaa.....
**********
Irine aliondoka kwa kasi kwa kuwa alikuwa amemuona mama yake ila kabla hajafika mbali akiwa karibu yangu nilimwambia,
"Saa moja jioni nitakuja nitakaa hapo kwenye kibanda cha chipsi,
Irine hakuitikia ila alinisikia nilijalibu kuangaza kuona kama nitamtambuwa mama yake ila sikufanikiwa kwa kuwa niliwaona wadada wawili wakiwa wamejazia matako wakiwa nje ya geita irine alipofika getini aliwasabahi kisha akaingia ndani,
*irine ameniambia mama yake au kaniambia kamuona dada yake?.*
Jioni mida ya saa moja nilirudi maeneo ya akina irine nikanyoosha mpaka kwa kumuuza chips,
"Man vipi?
"Poa mwana karibu, "asante, sasa kabla hata sijakaa nilikuwa naomba nikuulize,
"Uliza,
"Unamfahamu irine?
"Ndio,
"Naweza kupata kweli mida hii?
"Inawezekana ila kama hakujui itakuwa ngumu maana kale katoto kana nyodo sana sijui kwa kuwa ni kazuri?
"Tuyaache hayo nitamoataje?.
"Mimi huwa nachota maji ndani kwao,
"Basi fanya mpango basi nitakujali kitu kidogo,
"Poa jembe dakika mbili tu nimwambie nani?
"Mwambie derick,
"Poa,
Muuza chips alitoka akaenda kuchota maji mule ndani akarudi,
"Anakuja,
"Poa,
"Kaka wewe ndio shemeji nini maana hata hajaniuliza kitu nilipomwambia derick tu akasema nakuja,
Gafla geti lilifunguliwa akatokea mtoto wa kike mwenye sifa za kila aina,
"Ioohhh derick,
"Vipi baby?
"Shwari,
Itaendeleaaaaa....
Like 300 tunasonga mbele saa 12 jioni

No comments:

Post a Comment