STORY: MKE MWEMA.
MTUNZI : Baujiti
NAMBA : 0742868019wasap.
Sehemu ya tano.
leo nimewaandikia ndefu msome mpaka mshindwe kuimaliza.
Usisahau kuwa like yako Ndio italeta mwendelezo.
Nilijifanya sioni nikaenda nikaa na Shemsa tukawa tunajisomea mpaka mwalimu alipoingia akaanza kutufundisha baadhi Dua na Hadithi na alipomaliza aliniita tukatoka kwenda kuongelea nje.
" Seif hakika najivunia kuwa na mwanafunzi kama wewe' kwani una maadili mazuri matendo yako ni mawaidha (darasa) tosha kwa wengine."
"Allah (mungu) anisaidie aniongoze nisilewe sifa."
"Amina' ila nataka nikushauri kitu kama hakitakukwaza."
"Ushauri kwangu ni wa dhamani wala siwezi kukwazika."
"Seif yule binti unayependa kuwa naye sana ni binti msitaarabu mtiifu na mcha mungu pia' ila nakuomba ujitahidi kupunguza mazoa naye ili shetani asije kuwatoa katika mstari' sijui utanielewa?"
" Nimekuelewa Ustadhi (mwalimu)."
" Usinifikiliye vibaya kukwambia hivyo Habib (rafiki yangu kipenzi)."
" Ustadhi (mwalimu) siwezi kukufikilia vibaya kwani ushauri unaonipa ni mzuri sana na wenye manufaa"
" Sawa basi kanisaidie kufundisha lile darasa na mimi niendelee na rafiki zako sawa?"
" Sawa."
Nilifanya kama nilivyoambiwa na mwalimu nikaanza kuwafundisha watoto waliokuwa chini yangu' nilifurahia kwani walikuwa wakinielewa sana na kushika kile ninachowafundisha.
" Ambaye bado hajajuwa kusoma Dua ya kabla ya kula ni nani tumcheke?"
*kimya*
"Wote mumeilewa na kuishika kichwani?"
" Ndio "
"Haya mmoja mmoja atakuwa anasoma ndio anaondoka kuelekea nyumbani ambaye atashindwa hataondoka mpaka aelewe sawa?"
"Ndio."
Nikiwa naendelea na kufundisha Ustadhi Hamisi alinifuata na kuniambia kuwa Kuna ugeni wa wanafunzi wapya ila wageni waliwahi kusoma hapo zamani sasa ili kuendelea na darasa walilokuwepo nikasikilize wanisomee wakiweza waendelee na darasa la mbele wakishindwa wabaki humo.
" Umenielewa Seif?"
" Ninekuelewa."
" Usiogope rangi eti kwa kuwa ni wahindi."
" Nitasimamia haki."
"Sawa basi wacha niwambie waje kwako."
" Sawa."
Nilirudi darasani nikiwa nafundisha walikuja wakanisalimia kwa heshima japo nilikuwa nalingana nao kati yao mvulana mmoja alionesha heshima mpaka nafsi yangu ikawa na hofu hofu ila nikashindwa kujua ni hofu ya nini?
Walisoma kuanzia mwanzo ila nikabaini wanajuwa ila wakawa wamesahau vitu vichache.
" Wageni wangu naona mko vizuri kiusomaji ila kuna baadhi ya vitu mmesahau itabidi tuwe wote humu kama siku mbili tatu kisha mtaendelea na darasa mlilokuwa mumefikia."
" Sawa."
Walikuwa ni alikuwa ni binti mmoja wa kihindi na kaka zake wawili.
" Sasa na nyie simeni ile Dua kabla kuanza kula muiweke kichwani kwani atakaye shindwa tutabaki naye humu humu nikienda kula nyumbani tutakwenda kula naye pia kisha turudi naye tujumuike na wengine watakao kuwa wametoka manyumbani kula na kusalimu wazazi"
" Sawa."
Walianza kuisoma na kwa dakika 45 zilizokuwa zimebaki na baada ya kengelele kugongwa nilianza kuwasikiliza mmoja mmoja katika wanafunzi 30 walibaki kumi ambao walikuwa hawajaishika kichwani miongoni mwao walikuwemo wale wahindi.
" Jamani nyie ndio mumebaki endeleeni kusoma mpaka muelewa muishike kichwani hiyo Dua ndio mtaondoka sawa."
"Sawa."
Walisoma wakabaki watoto Binti wa kihindi na wavulana wawili na msichana mmoja.
Nikiwa darasani usitadhi Hamisi alikuja akaniuuliza sababu ya kuwepo mpaka muda huo nitamwambia akasapoti.
""Ni wazo zuri hongera sana."
Baada ya kuona hawaishiki Dua kichwani nilikwambia waende nyumbani ila jioni wakirudi wahakikishe wameiweka kichwani.
Yule binti wa kihindi aliyeitwa Zureyiha alinyoosha mkono kuashiria kuna anachotaka kusema.
"Zureyiha unasemaje?"
" Ungetekeleze ulichosema mala ya kwanza ingependeza zaidi kwa kuwa kufikia jioni tutakuwa tumeilewa."
Nilimuangalia usoni kisha nikawambia wote.
" Haya wote twendeni kwetu tukapate riziki kisha turudi ila kabla ya kwenda tuswali kwanza kwani muda wa ibada umefika."
" Sawa."
Tuliswali baada ya kuswali niliongozana na wanafunzi wote wa watano. Zureyiha, Jasmini, na wavulana watatu Haruna, Rashidi na kasim. Kwenda nyumbani.
Tulifika nyumbani baada ya kufika mama alitupokea akatutandikia jamvi akatupatia maji ya kunywa kisha akaniita pembeni.
" Sasa mwanangu mbona ugeni huu niagafla tutaurisha nini?"
" Leta kilichopo mama yangu kitatusha."
" Mwanangu nimepika ugali ila mboga nimechemsha maji ya moto nikatia chumvi ili kujaribu kuleta radha ya mchuzi."
"Tupatie hivyo hivyo mama yangu."
" Lakini mwanangu usijiringanishe na wale' wale ni watoto wa matajiri hawakiwezi chakula hiki?"
" Wote tumeubwa kwa udongo na wote tuna dhamani mbele ya mungu Kwa hiyo kilete kitakaye mshinda atakula akirudi kwao."
" Sawa."
Nilirudi jamvini mama akaleta chakuka akatunawisha tukaanza kula ila ya kumeza hata Tonge la tatu nilishituka kusikia napigwa teke la mgongo nikalia maamivu huku nikitaja baadhi ya majina ya mwenyezimungu kati ya yale 99.
" Yaani wewe ndio wakuleta watoto wetu kuwalisha taka taka?"
Walikuwa ni wazazi wa wale wanafunzi kumbe baada ya kuwakosa watoto wao walipouliza madrasa waliambia niliondoka nao kwenda kwetu wakanifuata kwa hasira wakapitia polisi wakapewa polisi watano wenye siraha utazani wanakuja kukabiliana na majambazi mzazi ambaye hakuwemo alikuwa ni mzazi wa Zureyiha ila wengine walikuja.
" Tunakuuliza wewe ni kuja kulisha watoto wetu uchafu huu?"
Walipiga ugali teke kisha wakaanza kunishambulia ila kumtaja mwenyezimungu sikuacha mpaka waliponinyanyua polisi kuniuliza sababu ya watoto wale kuwepo kwetu.
Niliwaeleza mwanzo mpaka mwisho ila wazazi hawakutaka kuelewa walizidi kusema kwanini nimewaleta wanao kula vyakula vichafu.
Walilifanya kuwa jambo ziko kutokana na kujua hali ya familia yangu ni ya kifukala' hawakufurahia watoto wao kuwa karibu na mimi si wao tu bali familia yangu ilikuwa inadhalaulika kuanzia ngazi ya Mtaa mpaka kitongoji kizima kwani sisi ndio tulikuwa mafukala kuliko wote.
Walinipiga ila polisi wakaingilia kati wakasema wasinipige tena wanipeleke polisi.
Waliniinuwa ila shati ilikuwa imejaa damu zilizokuwa zinanitoka kichwani mama alijaribu kunitetea ila akakutana pia na kipigo kutoka kwa baba yake na Jasmini' niliumia sana kuona hivyo mpaka nikasema kwa sauti.
"Mungu akulaani wewe kama kweli mungu yupo akudhalilishe anilipie kilio cha mama yangu na maumivu."
" wakikutuma mama utaleta huyu masikini kapuku ambaye hakukuandalia mazingira ya kuishi unaishi kama chokora unakula ugali na maji kama mbwa?"
Itaendelea..................
No comments:
Post a Comment