Thursday, January 31, 2019

SEBENE LA MAMA MKWE 1

Nakupa tamthilia moja hapa nchin.
SEBENE LA MAMA MKWE
1
MTUNZI. SEIF JABU
NAMBA. 0717394282
Endeleaaa......
Maisha ni safari ndefu japo hayasafiri kwenye gari,ndege wala treni, maisha yanakuwa ni safari ndefu kutoka na mawazo yako ya kutafakari ni jinsi gani utayamudu,
Duniani hakuna anayependa kibaya kila mmoja anapenda kizuri,
Naweza kuamini msemo usemao hakuna mwanamke mbaya dunia kwani unayemuona mzuri kwako kuna anayemuona mbaya kwake, na wewe unayemuona mbaya kwako kuna anaye mzuri kwake,
Maisha naweza kusema ni mwanake kwani bila mwanamke huwezi kuwa na furaha, nataka uwamini kila uonapo mafanikio ya mwanaume nyuma ya mafanikio hayo yupo mwanamke mh!!! Kuna wengine watabisha ila juwa ya kuwa furaha unayoipata kutoka mwenzi wako ndio juhudi yako ya kutafta maisha,
Ukiwa na mwamamke mwenye kero ndani ya nyumba basi kamwe huwezi kuwa na mafanikio ya kuridhisha kwani utatumia mda mrefu sana kumfikilia na kutafakari nini ufanye ili kureta usawa ndani nyumba mda huo unaoutumia kumtafakari ni mda wa hasara kwako,
Sitaki kukumbuka mengi yaliyomkuta kaka yangu george kutoka mikoa kusini,
George alikuwa mshauri wa watu mwalimu wa watu wa kila lika, ushauri wake siku zote aliwashauri wanawake na wanaume ya kuwa mpendane muheshimiane ndio nguzo ya maendeleo ndani ya nyumba,
Mnapokoseana mmoja ajishushe ili kuleta amani ndani ya nyumba na nyumba yenye amani siku zote inakuwa na baraka na mafanikio mengi sana,
Oooohhh george sikujua kama siku ndio darasa lako la mwisho kwetu kwani tulipoachana hapo nilirudia kukuona ukiwa katika sehemu ya kuhifadhia maiti mwili wako nilishiriki kuuosha niliumia kila nilipoona jeraha katika tumbo lako,
Jeraha lile lilinirudisha kufikilia nyuma kipindi kile unaniambia,
"Derick ukikosea kuowa juwa umekosea maisha, ukikosea kuowa juwa umeikosea dunia, ukikosea kuowa juwa umewakosea wazazi, ukikosea kuowa juwa umewakosea watoto wako, ukikosea kuowa juwa umewakosea ndugu zako, ukikosea kuowa juwa umewakosea majir

No comments:

Post a Comment