*KWA NINI WANANDOA WA KIAFRIKA SIO ROMANTIC?*
Ndoa nyingi ni kwa ajili tu ya *kulala na kuamka, kulea watoto na kuzeeka* pamoja mpaka kifo.
Wanandoa wengi ni mara chache sana kupeana *busu* na kukumbatiana wanapopata habari njema.
Mume humuwekea mkewe chakula *mdomoni* pale tu mke anapokuwa *mgonjwa* akawa hawezi kujilisha.
Ukimuona mwanaume *anamfungulia mlango* mkewe basi ujue mlango huo ni *mbovu* au una kasoro.
Kitu pekee kinachomfanya mwanaume wa kiafrika kuigusa *shingo* ya mkewe ni pale mke huyo anapolalamika kuwa ana *homa*. Hatoigusa tena mpaka atakapopata homa nyingine.
Muda pekee ambao *atambeba* mkewe mikononi mwake ni pale anapojifungua.
Ukiwaona *wamekaa nje* wakati wa usiku, usifikiri wanaenziana. Wanasubiri tu *harufu ya dawa* waliyopulizia ndani iishe.
Wanawake wengi wanawanunuliza *zawadi* waume zao pale tu mume anapokuwa *mgonjwa* hospitalini.
Muda pekee ambao *wanakimbia pamoja* ni pale inapotokea *hatari* na kila mtu akawa anakimbia.
Muda pekee *wanaokaa pamoja* jioni ni pale wanapotaka kwenda *kupeleka malalamiko* kwa wazazi wa mtu aliyempiga mtoto wao au aliyempa mimba binti yao.
Muda pekee *wanaokoga* pamoja ni pale wote *wanapochelewa* kwenda kazini.
Muda pekee ambao mke huyatazama kwa ukaribu *macho* ya mumewe ni pale jicho la mume linapopatwa na *uchafu*.
Kwa bahati mbaya, Waafrika wana mawazo kuwa kila mwanaume *romantic na mbembelezaji* anakuwa ametawaliwa na mke. Hapo wataanza kueneza umbea na kuzusha kua mke kampa *LIMBWATA* mumewe na si ajabu mwanaume huyo kuitwa *LOFA* au *BUSHOKE*.
*Tubadilike jaman, tujitahd kuzfanya ndoa zetu kua mpya kila uchao.........Na kwa wale tusiojaaliwa kupata bac tuwe na subira na tuyatekekeze haya mara tyu ya baada ya kupata kilicho halali kwetu*
No comments:
Post a Comment