HATIMA YA MAPENZI
MTUNZI..............KENDRICK LINCOLN JR.
SEHEMU YA THELATHINI ( 30 )

ILIPOISHIA..
Niliendelea kuangalia TV na baada ya muda Grace alikuja kuniita nikale chakula. Nilienda dining room na kuanza kula nikiwa nipo peke yangu. Ila nilikua nashangaa Grace pilika pilika haziishi kila muda anakuja huku akiwa ananitazama sana usoni..

ENDELEA..
Nilijiuliza sana atakua ana tatizo gani maana sio kawaida yake kabisa kufanya vile. Nikatamani nimuulize ana tatizo gani ila nikaamua nimpotezee tu. Nilikula na kumaliza kisha nikaingia chumbani kwangu. Nikaanza kuchat na Vanessa pamoja na Agness wote kwa wakati mmoja. Pia nilikusudia baadae Agness asinitafute tena ili nipate muda mzuri wa kuongea na Vanessa. Kama kawaida yake Agness hakuacha kunilaumu kuwa nimebadilika sana sina muda na yeye na nilisingizia kazi zinanibana sana. Nilimpa maneno ya kumfariji lakini ukweli ni kwamba sikua na muda nae kabisa kwani sasa hivi Vanessa ndo alikua ameiteka akili yangu. Kweli baadae nilimpigia simu Vanessa na tuliongea sana mpaka usiku mwingi huku bwana mkubwa akiwa amekasirika balaa kutokana na sauti yake kuwa inanipa mshawasha wa hali ya juu.

*************** ***************
Ilipofika wikiendi siku ya Jumamosi jioni, nilitoka out na Vanessa kama tulivyokubaliana. Nikampeleka mpaka fukwe za White Sands Hotel & Beach Resort na alionekana kupapenda sana.
Wow! This place is so beautiful ( Hii Sehemu Ni Nzuri Sana) yani sijawahi kufika hata mara moja.
Alinichanganya na viingereza vyake ila nikajifanya kama vile nimemuelewa ili asinione kila kitu nipo nyuma.
Mimi nimefika mara moja tu hapa kabla ya leo na nilikuja na wale marafiki zangu uliowaona siku ile kule Club Next Door.
Okay, ni pazuri sana sio siri nimepapenda.
Nikajiona kidume sana kumleta sehemu Vanessa na akaisifia kiasi kile maana kwa msichana wa kisasa kama yeye anakua ameshafika sehemu nyingi sana hivyo hata ukimpeleka baadhi ya sehemu inakua ni kama marudio tu kwake.
Tuliagiza vyakula na vinywaji vya gharama sana na baada ya kusubiri tuliletewa, vyakula vikiwa ni bado vya moto kabisa. Tulianza kula na kunywa taratibu huku tukiendelea na maongezi. Vanessa akaanza kuleta mahaba ya kulishana pamoja na kunyweshana na ilibidi na mimi nimlishe kama yeye. Muda wote alikua anapiga picha tu kwani Vanessa alikua anapenda picha kupita maelezo yani kila atakapokaa basi ni lazima atajifotoa tu.
Baby vipi kuhusu suala la kule tulipopata nyumba ya kuishi?
Hilo tayari limekwisha baby maana kitu kilichokua kinasubirisha tayari nimeshakimaliza hivyo kesho tutaenda wote mimi na wewe kwenda kulipa kodi ya miezi 6 kwanza.
Sawa baby nafurahi sana kusikia hivyo maana nilikua naona upo kimya wasije wakampangisha mtu mwengine ile nyumba ni nzuri sana.
Hawawezi kufanya hivyo yule mwenye nyumba huwa nawasiliana nae mara kwa mara na tayari nimeshamwambia kuwa kesho tunaenda kumlipa hela yake ya kodi.

Vanessa alifurahi sana na kuyafanya mashavu yake yatengeneze vidimpozi kama kawaida. Tulikula na kumaliza na tukaamua kuhamia upande wa swimmimg pool ili tukaogelee. Vanessa alienda washroom kubadilisha nguo zake na mimi nikaenda upande wa wanaume na kubadilisha nguo zangu na kuvaa kaptula fupi sana ambayo tuliinunua pale pale muda mfupi uliopita pamoja na vinguo vya Vanessa alivyoenda kubadilisha. Niliwahi kutoka na kumsubiri Vee kwa nje na baada ya dakika kadhaa alitoka na kunifanya nitoe macho utadhani mjusi amebanwa na mlango. Shape yake ilikua sio ya kawaida kwani alijazia hips sio mchezo huku tumbo lake likiwa dogo na limenyooka mithili ya ubao. Kitovu chake kilikua kidogo sana na kimeingia kwa ndani kidogo yani kama kimetengeneza kishimo cha kiaina. Kifuani sasa ndo alikua anaweza akawapiga watu shambulio la kijinsia kwani alikua na matiti mazuri sana yani bado yamesimama vizuri na makubwa wastani. Ukichanganya na nywele zake ndefu nyeusi za kibantu, Vanessa alionekana alikuwa ni zaidi ya mrembo na kunifanya nijivunie sana kummiliki mtoto mzuri kama yule. Vanessa alikua bado mbichi sana kwani aliniambia kuwa ana umri wa miaka 24 wakati mimi nikiwa na umri wa miaka 26. Yani ukimtazama umri wake na umbo lake unaweza usiamini kwani alionekana ni dada kabisa anakaribia hata miaka 30.
Wow! You look so good baby without t-shirt.(Unapendeza Sana Baby Bila Tisheti)
Sikumuelewa hata kidogo na nilibahatika kusikia neno tisheti tu hivyo nikabaki najiuliza tisheti itakua imefanya nini.
Eeh! Unasema tisheti imefanya nini?
Vanessa alibaki anacheka tu kisha akaniambia.
Mume wangu inabidi nianze kukufundisha Kiingereza maana ipo siku utanitia aibu sehemu. Haiwezekani kijana mtanashati kama wewe na mwenye pesa zako uwe haijui hata haya maneno ya kuombea maji.
Nilibaki nacheka tu huku nikiona aibu. Nilijuta kwanini wakati nipo shule nilikua natoroka na kwenda kuangua maembe maana sasa ndio nilikua naona faida ya yale niliyoyakimbia. Sio siri hata mimi mwenyewe nilishaanza kuona haja ya kujifunza kiingereza maana kwa kazi yangu ninayoifanya huwa ninakutana na watu wa aina tofauti tofauti na kuna muda nilijikuta nakwama na kuomba msaada kwa watu wa pembeni wanaoijua lugha.
Tulishikana mikono na kuanza kuelekea kwenye swimming pool huku watu wengi wakiwa wanatukodolea macho sisi haswa Vanessa. Vanessa hakujali kwani ndo kwanza alikua akiniwekea mara mkono wa kiunoni mara ahamishe aweke begani. Hakuona aibu hata kidogo linapokuja suala la mapenzi kati yangu mimi na yeye.
Tuliingia kwenye swimming pool ambapo Vee alikua ni muoga sana wa maji ila nilikua namfundisha kutokana na mimi kuwa mzoefu sana wa kuogelea kwani nilishawahi kufanya kazi ya uvuvi miaka ya nyuma.Ile siku tulifurahi na kula bata sana hadi usiku ambapo nilimrudisha Vee sehemu anayoishi.

Baada ya wiki moja mimi na Vanessa tukaanza kuhamia rasmi kwenye nyumba tuliyoipata maeneo ya Sinza. Nilinunua vitu vichache sana kwani tayari Vanessa alishakua na kitanda kizuri, kabati la nguo, TV kubwa ikiwa na ving'amuzi vyake pamoja na deki, dressing table na fridge kubwa. Niliongezea kabati la vyombo, masofa ya kisasa kabisa, mazulia makubwa ya manyoya pamoja na vitu vyengine vingi vyenye umuhimu. Rafiki zake Vee, Naima na Aisha nao pia walikuwepo siku hiyo tuliyohamia na walikua wanatusaidia kupanga vitu ndani. Marafiki zangu hawakuweza kufika kutokana na kutingwa sana na majukumu ya kikazi hivyo niliomba msaada kwa vijana niliowakuta mtaa huo huo na kazi ilipoisha niliwapoza na hela ya soda kama unavyojua maisha yetu Watanzania.
Pindi nilivyorudi nyumbani Mbezi Beach ili nikabebe nguo zangu zote pamoja na vitu vyangu vyengine nikakutana na Janeth ambaye nilikua bado sijamuaga. Tulisalimiana na akaniuliza kulikoni mbona nina haraka kiasi kile.
Samahani Janeth kwa kushindwa kukutaarifu mapema ila yote hiyo imetokana na kukosa muda mzuri wa kuongea na wewe. Unavyoniona hapa nimekuja kuchukua vitu vyangu na ninahama humu ndani.
Alex, kwanini lakini na imekua ghafla kiasi hiko?
Sio ghafla kaka David anajua siku nyingi tu kuhusu jambo hili na nilitegemea labda itakua amekwambia. Pia niliogopa nikikwambia unaweza ukapaniki hivyo ndo maana nikaona nisubiri hadi dakika za mwisho.
Alex jamani sio vizuri hivyo, umepata mwanamke eeh?
Janeth alikua na wivu na mimi kupita maelezo utadhani hana mume vile.
Sitaki nikufiche kitu Janeth, ni kweli nimepata mwanamke na nitakua nikiishi nae.
Nilijua tu mimi. Sasa mimi itakuaje lakini si unajua kama nakutegemea wewe.
Janeth please, naomba haya mambo kuanzia sasa tuyasitishe kabisa. Kusema ukweli siwezi tena kuendelea kumkosea David moyo wangu unanisuta sana.
Aleeeex, please. Nitaishi vipi mimi bila wewe.
Sikuamini nilipomuona akiwa anaongea hadi analia na nikaona sasa anafika mbali. Nilimfariji sana lakini hakunielewa hata kidogo na akaniambua kuwa atapigania penzi langu kwa gharama yoyote ili maana alikua hayupo tayari kuona utamu ninaompa unafikia mwisho. Janeth alinichanganya sana na niliamua kuingia ndani na kukusanya vitu vyangu vyote na kuvipakia kwenye gari kisha nikaondoka.

Usiku baada ya chakula nilikaa na mpenzi wangu Vee tukiwa tunaangalia tamthilia kwenye king'amuzi cha Azam.Tulikua tumekaa kimahaba sana huku Vee akiwa amenilalia mapajani kwangu na miguu ameiweka juu ya sofa. Mara nikamuona anageuka na kunitazama kisha akaniambia akaniambia.
Alex mume wangu sema unataka nini kutoka kwangu...............JE NINI KITAENDELEA?

USIKOSE KUFUATILIA SEHEMU YA 31 SIKU YA KESHO.
HADITHI HII IMEFIKA MBALI SANA HIVYO KWA ATAKAYEHITAJI NIMTUMIE INABIDI ALIPE SH. 200/= KWA KILA KIPANDE KIMOJA. AU LIPA SH. 1500/= BADALA YA 2000/= NIKUTUMIE SEHEMU YA 31 HADI YA 40.
NAMBA YA KULIPIA NI TIGOPESA 0719061143 JINA ALLY RASHIDI.
UKISHATUMA PESA HAKIKISHA UNANITAARIFU.
UKISHATUMA PESA HAKIKISHA UNANITAARIFU.

No comments:
Post a Comment